Thursday, November 28

Cha mchana cha wikiendi kutoka Kunduchi Beach Hotel

  Kama tulivyoahidi tutamalizia kuwaonesha ni menu gani ya mchana tulipata pande za Kunduchi beach Hotel, sasa ndo tunawajuza leo.
   Tunaomba radhi kwa kutokuwepo hewani siku mbili hizi kwa sababu zilizokua nje ya uwezo wetu, lakini baada ya yote tumerejea tena tukiwa tayari kwa kuwaletea mambo matamu kama ilivyo ada yetu.
  Mchana wa Jumamosi ile, tulikutana na menu hii: kulikua na samaki kaanga, mboga za majani, kuku aliyerostiwa huku vikisindikizwa na black olives na vipande vya pickles. Hii ndio sahani yangu niliyoamua ni nini kiwepo. Ila kwenye buffet kulikua na aina mbalimbali za menu za kujichagulia yaani wewe tu na mapenzi yako.

   Upande wa desert nilichukua yalojiri kwenye sahani hapo chini, amapo kuna vipande vya keki zilizotengenezwa na jibini, chokoleti, cocoa na vanilla, huku vingine vimenyunyuziwa syrup ya chokoleti na strawberry, pamoja na kipande cha chungwa.
    Leo ni Alhamisi, yaani Ijumaa mupya..... na inamaanisha wikiendi ndo inaanza.... Je, umjipangaje... karibu kulike page yetu k wa facebook ambayo ni www.facebook.com/MenuTime au tufwate kwa instagram @menutimes na twitter @menutimetz

No comments:

Post a Comment