Wednesday, October 23

Cha mchana cha Jumatano

   Mchana ulipofika, tukaitana na kukaribishana cha mchana ili siku ipate kuendelea vyema bila ya shida ya utupu wa tumbo. Eneo lilikua Kinondoni, nyuma ya jengo la Airtel kuna kijibar flani hivi, wapo vizuri kwenye swala zima la kitimoto na hapo chini ndo menu tuliyopata leo

  Wanaichanganya na mchicha flani kisha inaungwa kwa mbwembwe ila mwisho wa siku utamu upo. Bei pamoja na ndizi inagharimu 11,000/- tu za kitanzania.
   Tujuze mchana unapitaje pande ulizopo.....

No comments:

Post a Comment