Thursday, October 24

Froyo... Frozen Youghurt za kuleeee Quality Center

   Katika pitapita zetu, tulikatiza kule chan'gombe, palipo Quality center, na ghorofa ya juu tulipishana na sehemu yaitwa Froyo, wao ni wataalamu wa kutengeneza frozen youghurt. 
 Unajipimia mwenyewe youghurt uipendayo aidha ladha ya ndizi, chokoleti, vanilla na strawberry. Na iwapo wapenda viwe mixer ni rukhsa pia yaani chaguo ni lako.
Kisha wajiongezea vikorombwezo uvipendavyo wewe, kuna chokoleti zilizosagwa katika mitindo kadha wa kadha, pipi, toffee na mengineyo. Halafu kuna vipande vya matunda mbalimbali kama maembe, strawberry, ndizi, kiwi, n.k yaani wewe tu na utakavyo. Ukimalizia na syrup uipendayo kati ya vanilla, chokoleti au strawberry. Unapimiwa kiwango ulichochagua, unalipia na kuanza kufaidi utamu.
   Chini  nakuonesha mfano tu

  Baada ya uchaguzi wote na kulipia, hii ni froyo tuliyoonja. Na tamu na ilitugharimu sh 9,000/=. Yaliyomo humo ndani ni pamooja na yoghurt mixture zote nne, matunda aina 3, pipi na msagiko wa chokoleti na syrup aina 2.
   Nenda wajulie hali..... Onyo.... Waweza kuwa addicted maana ni tamu sana. Sisi tumeshakuwa addicted. Tutakua twawatembelea mara moja kwa wiki.
Kutoka Quality Plaza, Ljm nakujuza!!

No comments:

Post a Comment