Kuna msemo unaojulikana sana kitaani unaosema "kula bata hadi kuku askie wivu", kwetu ilikua tofauti kidogo maana sisi hatukuwa na bata bali tulikua na kuku na tuliwala kweli kweli.
Sasa hawa vyuku walimarinetiwa wakiwa nchi kavu hadi walipofika kule kisiwani ambapo walikutana na makaa ya moto yapo tayari kwa kuwachoma, kuwaivisha na kuliwa na wageni waalikwa.
Hatujapata kujua ni viungo gani viliwekwa humo (siri ya mpishi) , ila kihalali walikua watamu kuliko maelezo. Na kwa picha za vyuku hawa wanaochomwa, umepata kujua ni nyama gani zililiwa siku hiyo pande za Mbudya. Kulikuwa na salad kadhaa pamoja na wali mweupe katika kusindikizia msosi mzima.
Shukrani kwa uongozi mzima wa Mbudya, pia kwaTravor aliyetupikia, pamoja na Rafiqs wote tuliokuwepo pamoja na kufanya siku hiyo kuwa nzuri yenye kumbukumbu.
Twawatakia wikiendi njema sana Rafiqs!!
No comments:
Post a Comment