Thursday, August 22

Nyama choma njiani Iringa

  Pengine ni sababbu ya kuwa na uasili wa kichaga ndani yetu ndio sababu kuu ya kupenda sana nyama, na hii inakua kama umeridhishwa na wazee wa uchaggani. Hii tulithibitisha safari nzima ya Iringa, kuanzia tulipotoka Dar hadi tuliporejea. 
  Njiani ukimaliza mkoa wa Morogoro, kuna sehemu wanachoma nyama kwa ubunifu wa hali ya juu, na ukiondoa nyama pia wana visindikizio kama ndizi mzuzu za kuchoma na kukaanga, wali wa nazi, salad n.k, tuliambiwa paitwa Mvumero.
  Wakati twaenda, kwa kweli camera ilisahaulika, ila wakati twarudi tukasema lazima tuhadithie tukiwa na ushuhuda, na ushuhuda wetu ndio huu.
 Tuliagiza ndizi mzuzu za kukaangwa maana za kuchoma zilikua zimeisha, tulikua wengi ila zilitutosha. Ndizi ushuhuda wake ndo huo.

  Hizi nyama hazina viungo vingi sijui kuwa marinated na nini na nini na kadhalika, hapana!! Zina chumvi tu kwa mbali mno, kisha zachomwa taratiibu.

  Baada ya kuchagua mishkaki utakayo, itakayokutosha, pembeni ndo wakatiwa vipande vidogo vidogo, vikiongezwa chumvi kama utapenda, na ndimu kiasi tayari kwa kuliwa

  Tukahoji, mbona harufu yasikika sana ya utamu, yaani ule umbuzimbuzi unasikika sanaa, tukaambiwa huwa wanatumbukiza aidha mkia wa mbuzi au mguu ndani ya jiko, kama ionekanavyo kwenye picha kulia palee, ili harufu isafiri na kuita walaji. Tulikubali ujuzi huu na kushukuru kwa tips

   Tumebakiza siku moja tu ya kuongelea Iringa au safari yetu ya Iringa, na kesho tuna kitu kizuri cha kushare nanyi.

No comments:

Post a Comment