Wednesday, August 21

Mashine ya kukatia viepe

   Baada ya kufanya yetu yaliyotupeleka Iringa, tulipata wasaa wa kuzunguka Iringa mjini pale, na tulipishana na wananchi au tuseme wafanyabiashara ambapo kilichotuvutia zaidi ni hii mashine yao wanayotumia katika kukatia viazi vitoke vipande vidogo vidogo, vijulikanavyo kama chipsi a.k.a viepe.
   Tuliyemkuta alisema bosi amenunua mashine hii kutoka Kenya.
Ukiangalia hii mashine imeunganishwa na hiyo meza yake, kwa juu ikiwa haitumiki na imefungwa inaonekana kama ilivyo hapo chini pichani

  Hatua ni kwamba, unaweka chombo chini ili kuchota viepe vitakavyo katwa, kisha unafungua mashine na kuweka kiazi katikati kwenye meno ya mashine.

  Kiazi kitaonekana hivi, kikiwa katikati ya meno ya mashine tayari kwa kukatwa.

Mkono wa mashine unashushwa chini na ghafla vuwalaaaaaaa, kiazi kinagawanishwa vipande vipande, vikidondokea kwenye chombo ulichoweka hapo chini

     Tayari kiazi kimeshakatwa na kwa kufanya hivyo mfanyabiashara unaokoa muda wa kukata vipandevipande, pia unakua hauchoki sana.

  Baada ya somo, tukaona ni vyema kama tukimalizia na chipsi mayai a.k.a zege, ambapo pembeni kuna salad ya kabichi iliyopikwa na ingine ya kukwaruzwa, huku tukisindikizwa na mshkaki, na kikorombwezo cha chachandu a.k.a pilipili kwa mbali.

  Tulikuwa wanatimu wawili kutoka Menu Time, tukashauriana ati tule sahani moja pamoja, ilipoisha ikaagizwa ya pili, na ya tatu ndo tulipotosheka kwa utamu. 
   Hongereni sana wana Iringa kwa kuwa wabunifu au tuseme kwa kujiendeleza kutafuta urahisi na matumizi mazuri ya muda katika biashara zetu za chakula.
   Tuwatakie Jumatano njema, lakini kumbuka wiki nzima tunaongelea tuliyopishana nayo mkoa wa Iringa tulioutembelea wikiendi iliyopita.

No comments:

Post a Comment