Thursday, August 1

Futari ya Airtel

.... Baada ya kuona ya jana na juzi, twende kuona ya leo maana leo ndo twagusa zile menu zenyewe ziliwazo wakati huu wa mfungo wa Ramadhan. Karibu...
    Zilikuwepo tambi zenye usukari flani, zinaonekana ka zimekaangwa lakini zilikua laini na tamu muno.

   Magimbi nayo yalikuwepo, kwa macho waweza dhani yana ukavu flani, lakini si kweli, yalikuwa yanamezeka vyema tu

Mihogo iliyopikwa na tui la nazi na viungo nayo ilikuwemo. Ilikua na ladha ya pekee kwa kweli na hakika waliohudhuria watakubaliana na mimi

 Ndizi mzuzu ambazo zilipikwa kwa ustadi wake, zilizowekwa viungo kama iliki na vinginevyo, zikamaliziwa na tui la nazi zilikuwemo. 

Maharagwe yenye usukari kwa mbali na viungo nayo yalikuwepo ambayo yalisaidia kwenye vile vyakula ambavyo pengine vilionekana vina ukavu

   Rojo la nyanya chungu, viazi, njegere na mengineyo vikiungwa na tui la nazi nalo lilikuwepo katika kusindikiza menu nzima

  Vipande vya nyama ya samaki visivyo na ngozi vilikuwepo. Viliwekwa viungo kwa uchache sana na kukaangwa vyema kukamilisha menu ya siku hiyo

 Kwenye kila msosi, lazima salad iwepo. na kwa siku hiyo salad ilikuwepo kama inavyoonekana kuna karoti, maharage machanga, zucchini na mengineyo, na vyote vilichemshwa kidogo na kuongezwa pilipili manga kwa mbali.

 Njugu mawe nazo zilikuwepo katika rojo zitoo katika kuweka mambo ya menu yote yawe sawa.
Tumeona mpaka hapa jinsi gani Airtel walijiandaa vyema katika kufuturisha wageni wake, hakika walijipanga vyema. Tukirejea kesho tutaona visindikizio vya mlo wote a.k.a desert iliyoandaliwa siku hiyo ya Ijumaa. 
  tuwatakie siku njema leo hado tukikutana kesho.

No comments:

Post a Comment