Mama aliyejifungua anahitaji kula vyakula vyenye virutubisho vyote vinavyohitajika kutengeneza maziwa ya mtoto, maana ndo menu ya mtoto katika ile miezi ya kwanza mitatu na kuendelea. Hivyo suala zima la supu, uji, maji ya matunda, mtori na zaga zaga nyingine ziinahusika.
Kupika nimefundishwa na mama mzazi, hivyo muda huu wa yeye mama kumpikia mkwe wake yaani mke wa mwanae wa kiume, mie ndo nazidi kuongeza ufundi zaidi wa mapishi kwa kujifunza toka kwake na pia kula vitamu.
Moja ya mlo ambao lazima mama mtoto ale kila siku ni supu ya ng'ombe. Ntaja wafunza vyema namna ya kuipika ile inayotakiwa kwa mama aliyejifungua, pia ukienda kununua basi ununue upande upi ili upate ile supu inayohitajika, maana sio waenda nunua nyama tu kwasababu unanunua.
Kwa karibu yaonekana hivi, na vipande vya nyma kidogo
No comments:
Post a Comment