Wednesday, January 23

Picha toka kwa Rafiq - George

 George wa T.bonaz amesema ananza kula vyema, yaani vyakula visvyo na mafuta mengi na kuhatarisha afya yake pamoja na unene usio na mpangilio a.k.a diet. Moja ya kitu nachompendea George ni kwamba hata kama ni chakula cha aina gani anapika, lazima ataweka utundu wake na fleva za kutosha kumfanya mtu yoyote kutamani kukila chakula atakachotengeneza.
    Ni moja ya zawadi aliyopewa na Mola wake na anaitumia vyema. Siku si nyingi atakuja kutujuza namna ya kupika maini ni figo isiyo na mchuzi, ila kwa leo angalia menu aliyotayarisha ambayo yeyote anayefanya diet basi anaweza kuila na kupata utamu na ladha nzuri sawa na asiye na kufanya diet, yaani mwenye maamuzi ya kula menu yoyote pasipo kujali mafuta na vinginevyo.

   Hapo kuna maharagwe, salad na kipande cha kuku aliyeokwa. Waweza shushia na kimiminika chochote kisichokua na ulevi.
Kutoka Menu Time, tunakushukuru sana Geroge kwa kuendelea kushare nasi mapishi yako. 

No comments:

Post a Comment