Friday, January 25

Mapishi ya maini na figo yasiyo na mchuzi

  Kuna muda unasikia rafiq anasema hapendi chakula flani, mimi nadhani ni kwasababu ya upishi wa chakula hicho ndio kilichompelekea Rafiq kutokukipenda. Napenda kuwaambia marafiq kwamba ongeza ujuzi katika upishi, yaani kuwa na mipiko tofautitofauti ya menu unayopika hii haitamchosha mlaji, bali kuzidi kumpa hamu.
   George wa T.bonaz ni mbunifu katika mapishi yake, na leo anatujuza namna ya kupika maini na figo bila ya kuwepo mchuzi. Karibu tujiunge nae...


 Mahitaji:
  • Nyama ya maini na figo
  • Viungo (inategemea na unachopendelea kama kitunguu swaumu, viungo vya pilau n.k)
  • Nyanya
  • Kitunguu maji
  • Mafuta ya kupikia
  • Chumvi 
  • Pilipili
  • Zucchini
  • Beef cube
  • Karoti
Hatua
  • Tayarisha vyakula vyako kwa kukatakata vipande vya nyama, nyanya, kitunguu maji, zucchini na karoti



  • Ongeza viungo pamoja na chumvi ndani ya vipande vya nyama ili ladha iweze kuingia vyema

  • Weka mafuta kiasi kwenye sufuria, yakishapata moto, ongeza vitunguu na chumvi kiasi na vikaange mpaka viive
                                       
  •  Ongeza nyanya pamoja na karoti na zucchini katika vile vitunguu vilivyoiva jikoni
                                           
  •   Tumbukiza pilipili bila kuzikata, pamoja na beef cubes kisha endelea kukoroga mchanganyiko wa mboga ili uweze kuiva na kuchanganyika vyema
                                           
  • Weka vipande vya nyama ya figo na maini, kisha acha viive kwa pamoja, Usivifunike ili kuepuka utengezaji wa mvuko ambao utaleta rojo au mchuzi
                                   
  • Onja chakula chako kama kimeshaiva, tayari kwa kupakua na kuliwa.
                                    
   Waweza kula nyama hiyo iliyopikwa vyema na chakula chochote iwe wali, viazi vya kupondwa, ndizi za kuchoma, chipsi, ugali, mkate n.k yaani itategemea wewe una hamu ya kula mlo gani siku hiyo. 
   Kutoka Menu Time, tunamshukuru sana George kwa kushare nasi upishi huu. Iwapo nawe ungependa kutujuza namna ya kupika pishi lolote tuandikie kupitia menutimes@gmail.com au info@menutimetz.com

No comments:

Post a Comment