Saturday, January 26

K.A.B.L.E Inc & Menu Time yapanga kusambaza Upendo pale Malaika Orphanage Foundation - Dar

   Wiki moja toka leo, yaani siku ya Jumamosi tarehe 2 ya mwezi wa Pili, kuanzia saa 4 za asubuhi, wote mnakaribishwa kushiriki katika siku hii muhimu na watoto wa Malaika Orphanage Foundation, kilichopo Kinondoni Dar es salaam, ambapo timu ya K.A.B.L.E inc pamoja na Menu Time na marafiki wengine tutakuwepo.

   Ujumbe wetu ni huu: "Tujitolee siku hii kwa watoto hawa. Tujiunge pamoja na kutoa chochote tulichonacho katika kufanya mabadiliko katika maisha ya watoto wa Malaika Orphanage Foundation, aidha iwe katika kujitolea kwa nguo, muda, pesa, sabuni, chakula, vikaragosi au kivingine.
              
  Nia yetu ni kutafuta namna ya kupata pesa ya kununua bidhaa muhimu kwa ajili yao, pia kucheza nao, kula nao na kuipa umuhimu siku hii kwao, kwa kuhakikisha hilo basi, kuna fulana zenye chapa ya KABLE pamoja na BE YOU, DO YOU zinazouzwa kiasi cha shilingi 20,000/= ambapo pesa itakayopatikanika itatolewa katika manunuzi ya bidhaa muhimu kwa watoto wa Malaika Orphanage Foundation.
  Unakaribishwa kujumuika nasi katika kuleta mabadiliko katika maisha ya watoto wa Malaika Orphanage Foundation                           
    Iwapo ungependa kushirikiana nasi wasiliana nasi kupitia namba hizi, 0657 999 902 na 0715 999 790 au  tuandikie kupitia menutimes@gmail.com tujuzane zaidi.

No comments:

Post a Comment