Kubwa zaidi ni kwamba tutakua tunapata kuona menu mbalimbali toka pande hizo, ambapo Bwana Epphy atakua anaziwasilisha vilivyo.
Japo tulikua kimya kwa muda kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wetu, sasa tumerejea na mambo mema, mazuri, matamu na uzuri tumepata kuwa na wawakilishi pande tofauti tofauti, hivyo tunaamini mtaenjoy kuona hizo menu toka pande mbalimbali za dunia. Karibuni sana!!
Kwa kufungua kinywa, Bwana Epphy alitujuza kuwa alitayarisha mwenyewe mlo wote, na alishushia na chai ya maziwa, ambayo haikuambatanishwa kwenye picha.
Yaliyomo kwenye sahani ni mkate uliookwa, mayai na bacons.... Alisema waweza kushushia na kimiminika chochote sio lazima iwe chai kama alivyofanya yeye. Sasa uamuzi ni wako. .
Hope umepata hamu ya kujitengenezea mlo kama huo katika kufungua kinywa chako.
Kutoka South Africa a.k.a bondeni, Epphy anatujuza.
No comments:
Post a Comment