Saturday, January 19

Lasagna

   Moja ya mapishi ambayo hunivutia kupika au kuvila ni vyakula vya asili ya waitaliano. Naongelea macaroni, lasagna na kadhalika. Pengine ni kutokana na yaliyomo ndani ya vyakula hivyo, kimoja wapo kikiwa ni jibini. 
   Dar iliyo salama, ukiwa unapita pande za Seaview, kuna kituo cha mafuta chaitwa Puma, kuna restaurant flani yaani fast food flani, ambapo kuna mama wa kihindi anauza vikorombwezo vya aina mbalimbali. Kuanzia chachandu, mango pickle, pickle za mbilimbi nakadhalika. Ukiachia mbali uuzaji wa vikorombwezo hivyo, kama restaurant zingine kuna msosi pale, na moja ya msosi ambao unanifanya kufunga safari na kuufwata ni Lasagna. Sijajua kiswahili chake ni nini, ila ni chakula cha asili ya waitaliano.
   Ushuhuda wa picha wa Lasagna toka Fast food ya Puma pande za Seaview Dar ni hii

   Hiyo ni kiasi cha  mtu mmoja, na ukila washiba vyema tu. Nikasema tuikate tuone kwa ndani yafananaje?, na ushuhuda ndo huo hapo chini, wa picha lakini.

   Waweza shushia na kinywaji cha aina yoyote haswa maji ya matunda a.k.a juice, soda, maji baridi, maziwa au kingine ambacho sijakitaja ila wakipenda na waona chafaa kushushia msosi huu.
   Tuambie menu gani waipenda sana, na waipata wapi kupitia info@menutimetz.com au menutimes@gmail.com
    Kutoka seaview, LJM wa MT naarifu!! wikiendi njema ndo timu nzima ya MT tunawatakia.

No comments:

Post a Comment