Thursday, January 17

Picha toka kwa Rafiq - P. Richard

   Mara kwa mara huwa tunatumiana picha za misosi na P. Richard kupitia mtandao wa jamii yaani WhatsApp. Kwa makusudi namtumia vyakula vya nyumbani a.k.a Tanzania kwasababu najua yeye ni mpenzi mno wa menyu hizi, ila kutokana na umbali anavimiss mno. Sasa kumpunguzia mzigo wa mawazo, naamini picha zinamfariji, ili siku anapokuja kutembelea nyumbani aweze kuwa updated na mambo ya menu.
   Tatizo lake vile vyote vinavyomvutia kwa picha vinaandikwa pembeni, halafu akiwa dar, inatolewa listi kwamba atataka kuvila vyote ili kujua taste yake. Menu Time tunafurahi kuassist kwenye hilo. 
   Kwa upande wake, yeye ananitumia picha za menu za aina mbalimbali ambazo hupishana nazo iwe ni menu ya asubuhi, mchana au usiku. Kuna muda unaweza kufikiria kuvunja screen ya simu ili kupata kujaribu taste ya hiyo menu umetumiwa.
   Jana alituma picha hii

   Alisema ni Mexican food, jina hakumbuki vyema, yawezekana kuwa ni Chicken bowl. Humo ndani sasa kuna kuku, wali, mahindi, peco de galo na sauce.
   Kwa mtazamo kinaonekana kitamu flani. Hiki huliwa kama chakula cha mchana au usiku.
Asante sana P.Richard kwa kuendelea kushare nasi all the way from USA. 

No comments:

Post a Comment