Wednesday, January 16

Picha toka kwa Rafiq - Emma

   Siku za mwisho wa wiki a.k.a weekend, tulipokea picha inayoonesha chakula alichokula dada Emma Kokusima. Ndani ya barua pepe aliyotutumia aliandika kuwa "Hiki ni chakula changu cha mchana; kuna wali, sauce, samaki wa kukaanga na salad ".
   Picha tuliyopokea ni hii hapa......

   Ndimu na pilipili pembeni vinasindikiza msosi mzima alioupata Da Emma. 
Timu nzima ya MT tunasema shukrani sana kwa kushare nasi, japo hakusema ameupata wapi mlo huu ili Rafiq mwingine naye aweze kujua maeneo iwapo ataupenda na kutaka kuuonja.
  Rafiq, nawe karibu kushare nasi iwe ni picha au namna ya kupika pishi lolote, email address zetu ni menutimes@gmail.com au info@menutimetz.com 

No comments:

Post a Comment