Imetimu siku ya nne, tunaangalia upande wa Matunda ambayo anapaswa kuyala Rafiq aishiye na VVU. Na hii haimaanishi kwamba kwasababu hauishi na VVU basi hupashwi kuyala matunda haya, hapana.... ila tunawaelekeza vyakula bora mbavyo anapaswa kuvila Rafiq aishiye na VVU.
Vyakula aina ya matunda ni kama vifuatavyo:
Mapera, Machungwa, Maembe, Machenza.....
Mananasi, Picheli, Topetope, Mastafeli ......
Mapapai, Zambarau, Mafenesi ......
Malimao, Ukwaju na Ubuyu
Hayo ndo matunda yapaswa kutiliwa mkazo ulaji wake. Yapaswa kuangalia urahisi katika nyanja zote za upatikanaji wake, kisha kuweza kufanikisha upatikanaji wake na hatimaye kuliwa na Rafiq aishiye na VVU.
Kumbuka kuwa japokuwa tunawajuza ni vyakula gani yapaswa aishiye na VVU kuvila, haimaanishi kwamba aache matumizi ya dawa za kuongeza siku za kuishi (ARV's) iwapo anatumia. Pia ni wajibu wa kila mmoja wetu kujitunza, kujilinda na vilevile kuwatunza na kuwalinda tuwapendao.
Karibu kuchangia lolote kupitia info@menutimetz.com
No comments:
Post a Comment