Wednesday, December 5

Vyakula bora kwa aishie na VVU

    Tupo siku ya tatu, tunaendelea kufahamishana vyakula bora kwa Rafiq aishie na VVU, iwe anajipikia mwenyewe au tunamsaidia kutayarisha.
    Tulianza juzi, tumesema jana na leo tunasonga mbele, na siku ya leo tunaendelea kuangalia vyakula ambavyo ni muhimu sana kwa kila mmoja wetu ila zaidi kwa yule mwenye upungufu wa kinga mwilini, tukimaanisha yule aishie na VVU.
    Leo tunaangalia vyakula vya mbogamboga.
Hapa kuna:
Matembele, Mchicha, Majani ya maboga, Majani ya kunde,  Kisamvu, Figiri, Spinachi, Sukuma wiki, Mnafu, Mchunga .....



 

 Biringanya, bamia, karoti, maboga, matango, pilipili hoho, nyanya chungu na mlenda


                                          
Tunasisitiza kuwa angalia urahisi wako katika upatikanaji wa vyakula hivi. Iwe urahisi wa umbali wa kuvinunua, urahisi wa bei, urahisi wa upishi n.k. Mwisho wa siku vyakula vyote vilivyoorodheshwa vyapaswa kutayarishwa na kuliwa na yule Rafiq anayeishi na VVU.
Iwapo una maoni, wakaribishwa na iwapo kuna lolote la kuchangia basi karibu kututumia maoni yako kupitia info@menutimetz.com

No comments:

Post a Comment