Siku ya tano leo toka tumeanza kuhabarishana kuhusiana na vyakula bora mbavyo anapaswa kuvila yule Rafiq aishiye na VVU. Tunaamini vyote vime eleweka vyema hivyo inatupa moyo wa kusonga mbele na aina nyingine ya vyakula ambavyo wanapaswa kuvila wote waishio na VVU.
Leo tunaangalia Vyakula vyenye Mafuta na Sukari. Hapa tunaongelea:
Nazi, Mawese, Alizeti ........
Karanga, Ufuta........
Korosho, Mbegu za maboga, Kweme........
Siagi , Samli.......
Miwa, Asali, na Sukari
Tunaendelea kusisitiza urahisi wa upatikanaji wa vyakula vyenye mafuta na sukari ni juu yako wewe kuangalia wapi vitapatikana na kwa gharama ipi. Cha muhimu ni kuhakikisha kwamba vyakula vilivyoorodheshwa vinatumika na yule Rafiq mwenye kuishi na VVU, huku akiendelea kupata ushauri nasaha na kutumia vidonge vya kuongeza maisha iwapo ameanza kuvitumia.
Tukutane kesho katika kumalizia mada hii
No comments:
Post a Comment