Monday, December 3

Vyakula bora kwa aishie na VVU

 
   Tulisema tutakuja juzana ni menyu gani yapasa kula pale ambapo tunakumbwa na magonjwa mbalimbali. Hii ni kwa ajili ya kuweza kusaidiana ni chakula gani chapaswa kuliwa, muda wa kukila, faida zake na kadhalika.
   Wiki hii tutaangalia, je, ni menyu gani au aina gani ya vyakula anapaswa kuvila, yeyote aishiye na VVU yaani Virusi Vya Ukimwi.
   Sasa utaangalia urahisi wa kupata hivi vyakula ukiangalia vipengele vifuatavyo: ukaribu wa soko la kununulia vyakula, upatikanaji wa urahisi vya vyakula hivyo tutakavyovitaji, urahisi wa bei ya manunuzi ya vyakula hivyo pamoja na urahisi wa upishi na uhifadhiji wa vyakula hivyo. Kwasababu tunatofautiana mazingira yetu kwenye vipengle hivyo juu, basi chagua mojawapo ya aina ya chakula iliyo rahisi kwako itumie.
 Tutaanza na vyakula vya Nafaka, Mizizi na Ndizi.
   Hapa kuna:
Mahindi, Ulezi, Mchele, Ngano, Mtama, Uwele.....                                                                           
 

 


 
Viazi vikuu, Viazi vitamu, Viazi mviringo, Mihogo, Magimbi na Ndizi



 
   Leo, tumeangalia fungu la kwanza yaani vyakula vya Nafaka, Mizizi na Ndizi. Tutaendelea kuwajuza zaidi, kesho na siku zijazo.
   Iwapo una lolote la kuchangia, karibu kuacha maoni yako kwenye eneo la maoni hapo chini, au tuandikie kupitia anwani info@menutimetz.com


2 comments:

  1. asante dada kwa kujali afya zetu, Mungu akubariki. Nilikuwa naomba unisaidie jinsi ya kupunguza uzito bila madhara ama Diet nzuri kwetu sisi wanene.

    all the best

    ReplyDelete
  2. Asante kwa salamu, Mwenyezi Mungu atubariki sote. Nafanyia kazi ombi lako, na ili kukupatia mpangilio mzuri wa diet ni vyema kupata ushauri fasaha kutoka kwa wauguza na wakunga, na itakapokuwa tayari basi ntashare nanyi nyote.

    ReplyDelete