Sunday, December 2

Picha kutoka kwa Rafiq

   Tuna marafiq wengi toka pande mbalimbali za dunia, na wanatujuza ni menyu gani wanapata, wapi wanaipata na kama wanaipika wenyewe, basi wanaipikaje. Baada ya kujuzwa, nasi tunawajuza nanyi marafiq wetu wa Menu Time.
   Wikiendi hii, tumeletewa picha toka kule alipo raisi Obama, naongelea Marekani. Kutoka kwa Peter M Richard, alishare nasi picha ya sahani aliyojipakulia kama mlo wa usiku.
   Kwenye sahani kuna wali mweupe, kisamvu, vipande vya chipsi, ndizi mzuzu na kipande cha kuku..... mlo watamanisha sana huu!! karibu kuangalia
 
   Kutujuza na kushare nasi mlo uliokula, tafadhali tutumie kupitia anwani hii,  info@menutimetz.com nasi tutaonesha hapa. Karibuni sana.
Kutoka Marekani, tunamshukuru Peter!!

No comments:

Post a Comment