Sasa uzuri wa kujitangaza ni kwamba ukishaonekana, mteja atakutafuta ulipo pasi kujali umbali, gharama atakayotumia n.k ili mradi akupate na kuweza kujipatia hiyo bidhaa unayouza.
Yametutokea haya, ni hivi, katika pita pita zetu zetu za kila siku, tulikua tunapishana na tangazo la restaurant moja uliopo Mikocheni. Mara ya kwanza hatukujua ipo wapi restaurant hii, sababu tangazo lipo juu, barabarani halafu tulikua ndani ya gari linaloenda, hatukupata wasaa wa kusoma kila kitu zaidi ya jina la restaurant. Baadae katika kupita mitaa ya Mikocheni tukaliona tena tangazo hilo, tukajipanga, tukajitayarisha na jana tukawatembelea
Tunaongelea restaurant iitwayo Rodizio Brazilian Grill. Alessandro, ambaye ni mmiliki wa restaurant hiyo alitukaribisha vyema katika kupata chakula cha jioni. Karibu tusafiri pamoja....
Ukifika wakaribishwa na wahudumu wachangamfu, wachagua meza, wachagua kinywaji kisha wajipanga kula. Chakula cha usiku kinakuwa served kwa style ya buffet. Ukiwa tayari kwenda mezani kupakua ....... unakutana na kianzio a.k.a starter ya baridi na ya moto. Pia kuna wali, ndizi, mboga mbalimbali ambapo zote wajipakulia mwenyewe a.k.a self service.
Nakuonesha kianzio cha menyu nliyopakua mimi
Halafu unarejea kwa meza yako, waketi, unakua umepewa kikadi flani ambacho ukikiweka mezani na upande wa juu ukaonekana una rangi ya kijani, basi yamaanisha upo tayari kula nyama. Wahudumu wataanza kuja mmoja baada ya mwingine wakiwa na nyama tofauti tofauti na kukukatia vipande, wataendelea kufanya hivyo mpaka utakaporidhika kuwa umeshiba, utalazimika kugeuza kile kikadi kwenye upande wa rangi nyekundu, na hiyo itamaanisha usitishaji wa hudumu ya kukatiwa nyama na wahudumu.
Pichani chini inaonekana kiupande, mmoja wa wahudumu akiwa tayari kutukatia nyama, kwani vikadi vyetu vilionesha rangi ya kijani
Kuna nyama za aina nyingi zikiwemo jamii ya majini, ndege na kina ng'ombe, kondoo, n.k. Yaani wahudumu wako vizuri kwenye kuhakikisha unahudumiwa vyema na hauachwi peke yako. Kumbuka nyama zote zimepikwa kwa mtindo wa kubanika a.k.a grill.
Chini ni moja ya sahani yetu inaonesha vipande vya nyama tofauti tayari kwa kuliwa. Hapo kuna sausage, nyama ya mbuzi kipande cha samaki na kuku.
Kila mara sahani yako inapoonekana kama imetumika sana na kuchafuka, wahudumu wanaibadilisha kwa sahani safi ili uwe mwepesi kuendelea kula nyama mbalimbali.
Ukishabadilisha card kuwa ya rangi nyekundu, huku ukimaanisha umetosheka na nyama, kifuatacho ni desert, ambapo kwa jana ilikua ni nanasi lililobanikwa pia a.k.a grilled. Ila liliongezewa nakshi ya viungo kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini. Unakatiwa kipande ili kushushi mlo wako. (picha imegeuka kiupinde)
Radizion Brazilian Grill ni restaurant ya kujipanga kwenda, ili upate kuonja na kula nyama zenye ladha tofautitofauti, zilizopikwa kwa ustadi wa hali ya juu. Pia wahudumu ni wachangamfu, wako fasta, wanakusimamia kuhakikisha hupati usumbufu wa aina yeyote, yaani wapo kwa ajili yako. Inakua kama vile upo home flani hivi na ndugu zako.
Asanteni sana RBG, Asante Alessandro Panizzi ambaye ni mmiliki wa restaurant, Asante Da Joy ambaye ni mmoja wa wahudumu aliyetuhudumia na kutuzawadia tabasamu muda wote. Asanteni kutufanya tujisikie nyumbani. Asanteni Ephraim Musiba and Faraji Dumba kwa kukubali kwenda nasi!!
Kutoka Radizion Brazilian Grill iliyoko Mikocheni, Dar iliyo Salama LJM wa Menu Time naarifu.
No comments:
Post a Comment