Thursday, November 29

Ujumbe juu ya ukimya mwingi

   Tunasikitika kwa kuwa kimya na kutoweza kuwajuza yaliyojiri katika kipindi cha kama wiki mbili hivi. Tumekua na mambo mengi kidogo katika kuboresha Menu time. Sasa tuna mengi yanafanyika, na kuyajua tafadhali ingia kwenye website yetu yaitwa www.menutimetz.com.
    Pia tumejikuta tunatumia muda mwingi kuwajuza wapi tunapata vyakula vya kila aina, tukasahau kuendelea kufundishana namna ya kupika menyu mbalimbali. Baada ya kuliona hilo, tumelifanyia kazi na kuamua kuanzisha blog ingine ambayo itatujuza maeneo zaidi ili huku tubaki kupeana somo zaidi kuhusiana vyakula na yote yahusuyo jikoni.
   Blog ipo katika ngazi za mwisho kumalizika, na ikiwa tayari tutawajuza na sote tuendelee kuitembelea kujua yatakayojiri zaidi.
   Jiunge nasi kupitia facebook, tutafute Menu Time.
   Kwa niaba ya timu nzima ya Menu Time tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokea na tunawashukuru kwa kuendelea kuwa nasi na kwa kutuvumilia.
   Asanteni Rafiqs!!


  

No comments:

Post a Comment