Friday, November 16

Breakfast @ Mokka City!!!

   Moja  ya migahawa nimewahi kuongelea kutokana na upatikanaji wa vinywaji mbalimbali visivyokuwa na ulevi, naongelea juice, chai, kahawa n.k ni Mokka City cafe & lounge iliyopo Dar Es salaam. Ukiondoa vinywaji kuna vyakula vingi vitamu.
   Twende kuona waweza pata menyu gani ukifika hapo mida ya asubuhi. 
Hapo kuna croissant yenye ladha ya chokoleti kwa ndani, kisha juu yake imenyunyuziwa chokoleti.
 
Kuiona vyema ili upate kuimagine utamu utakuwa vipi, pia tumeonesha kwa pembeni inaonekanaje?
 
Kisha ilisindikizwa na Cappuccino one of my favourite drink.

Ukipata muda pitia hapo weekend hii, na upate kujaribu moja ya milo yao, kwani ni mitamu muno.
Menu Time inawatakia wikiendi njema na salama!!

No comments:

Post a Comment