Mahitaji:
- Nyama ya ng'ombe kilo moja (yaweza kuwa ya mfupa au steki)
- Chumvi kiasi
- Kitunguu maji 1
- Nyanya 2
- Viazi ulaya 2
- Pilipili hoho 1
- Karoti 1
- Pilipili manga kiasi
- Kitunguu swaumu kiasi
- Tangawizi kiasi
- Mafuta kiasi
- Chemsha nyama yako ikiwa umeikata vipande vipande, ongeza chumvi, kitunguu swaumu, tangawizi na pilipili manga. Ongeza maji kila inapokaukiwa na maji.
- Baada ya nyama kuchemka vyema, weka sufuria safi motoni, ongeza mafuta kiasi, yakishapata moto ongeza chumvi kiasi, kisha weka vitunguu maji acha mpaka viive. Ongeza vitunguu swaumu, tangawizi kiasi koroga mpaka viive. Ongeza pilipili hoho, karoti na vipande vya viazi ulaya, koroga na acha viive vyema.
- Ongeza nyama iliyochemka, acha viive vyema, kila inapokaukia ongeza supu iliyobaki kwenye nyama uliyochemsha. Baada ya kuchanganyika vyema, weka vipande vya nyanya na acha rosti ijitengeneze.
- Ongeza Royco au Onga kama unapenda, kisha malizia na tui la kwanza la nazi, ambapo utakoroga rosti yako kuhakikisha haikatiki inapochemka.
- Epua rosti yako tayari kwa kuliwa.
Jaribu pishi hili, kisha tujuze je, imetokeaje?? tutumie picha tushare na Rafiqs. Karibuni tuendelee kujifunza mapishi mbalimbali.
No comments:
Post a Comment