Tuesday, December 11

Shieni bar Menyu yazidi kukua sasa!!!

   Menu time katika kujiendeleza, kuimarika na pia kuwapatia wateja wetu kile chakula tumbo linapenda, Shieni bar ambapo Menu Time tumefunga kambi, tunatoa huduma za take away na hivi karibuni tutaanzisha delivery a.k.a kukufikishia menyu uliyochagua pale ulipo.
   Tutakuja kuwajuza menyu nzima inayopatikana hapo Shieni bar iliyopo Sinza, pia tutawajuza namba zetu kwa ajili ya kuwasiliana nasi kisha tuanze kukufikishia pale ulipo.
    Hii ni menyu ambayo Rafiq alitoa oda, kisha aliipitia kama take away. Yaitwa chipsi na  nusu kuku tamu. Kuku tamu hii hupikwa kwa kutumia mafuta ya kuku mwenyewe, yaani haiongezwi mafuta mengine. Nzuri sana kwa wale wasiopenda vyakula vyenye mafuta.
   Muonekano unakuwa hivi...
 
    Fanya kututembelea Sinza mori, Shieni bar, upate kuonja moja ya menyu za hatari zinazotengenezwa na Menu Time team.
    Wasiliana nasi kupitia info@menutimetz.com au +255 715 999 790

No comments:

Post a Comment