Monday, December 17

Macaroni na Sausages

  Leo tumepika macaroni na beef sausages, tukamalizia na jibini kwa juu kabla ya kuvioka pamoja. Hatua za kufuata ni zile zile, kwamba unapika macaroni na yakishaiva vyema unaweka pembeni. Kisha unachemsha sausages zako mpaka ziive vyema. Kama utakua na sosi yeyote wataka kutumia pia ni vyema kwani yaongeza ladha na utamu.
   Sosi zipo zauzwa supermarkets na zipo za aina tofauti, kuna zenye ladha ya uyoga, ya jibini, ya nyanya n.k ni kutokana na chaguo lako wewe. Sisi tuliamua kutumia yenye jibini, ambayo ilichanganywa na maziwa, na kitunguu maji kimoja na jibini zaidi ya kukwaruzwa.
   Baada ya kuvichanganya vyakula vyote yaani macaroni yaliyoiva, sausage zilizochemka, na sosi iliyokua tayari, takaweka kwenye chombo tayari kwa kuoka, halafu juu yake tukaongeza jibini zaidi.
   Na hii ndo picha ya menyu ilivyotokea baada ya kutoka kwenye oven...
 
Baada ya kupakua na kuweka tomato sosi, ilionekana hivi...
 
Haya macaroni ni tofauti kidogo, yana umbo la kujikunja na ndani kuna nyama au jibini. Yapo kwenye baadhi ya Supermarkets, ila tutakuja kuwajuza mengi kuhusiana na haya macaroni.
 
   Soma makala zilizopita kwenye Mapishi time kujua namna ya kupika macaroni, kama hukuwahi kujifunza pale tulipotoa somo. Tupo kwa ajili yako hivyo basi kuwa huru kutuuliza chochote kupitia contacts zetu.
   Tunawatakia wiki njema yenye mafanikio.

No comments:

Post a Comment