Tuesday, December 18

Chatini ya Karoti, Nazi na vitunguu

   Leo tumetumiwa mahitaji ya kutengeneza Chatini ya karoti, nazi na vitunguu. Hatukuelezewa hatua za kuipika hii chatini mpaka itokee kama picha ilivyotumwa, naamini mdau alikutana nayo sehemu, akaipiga picha baada ya kumvutia pamoja na utamu baada ya kuila, kisha akaulizia mahitaji gani yametumika katika utengenezaji kwa nia nzuri ya kushare nasi.
   Tutamtafuta Vincent na chanzo cha pishi hili ili kufuatilia hatua alizozifanya mpaka kupata hiyo Chatini kama inavyoonekana kwenye picha
   Wakati twasubiria hatua, tuangalie ni mahitaji gani yanahitajika katika upishi huu.....
Mahitaji:
  • Kitunguu maji kikubwa - 1
  • Karoti kubwa - 1
  • Nazi - tui lake kipimo cha nusu kikombe
  • Pilipili mbuzi kubwa - 1 au 2 (inategeme unataka iwe kali kiasi gani)
  • Kotmil - fungu 1
  • Rojo ya ukwaju kipimo cha nusu kikombe
  • Chumvi kiasi
Baada ya kuviunganisha viungo vyote, ambapo tutarejea kuwajuza tunaviunganishaje, kama ni kuvipika au kusaga tu, Chatini yako ya karoti, nazi na vitunguu maji itaonekana kama hivi:  

    Kama una ufahamu wa hatua za kupitia mpaka tufikie hapo mwisho karibu kushare nasi. Tuandikie katika menutimes@gmail.com au info@menutimetz.com nasi tutawajuza wengine.
    Vincent asante sana kwa kushare nasi kaka.

No comments:

Post a Comment