Baada ya bites tulizokaribishwa ambazo zilikua sambamba na vinywaji, tulikaribishwa ndani, kuweza kuanza shughuli tuliyoitiwa pale Golden TulipHotel .
Na muda wa msosi ulipofika, Menu Time ndipo tulipohusika zaidi. Kulikuwa na aina mbalimbali za vyakula, kuanzia salad, supu, nyama choma mpaka wali mweupe.
Bakuli zasubiria kuweka supu tayari kwa wageni kuenjoy
Kulikua na supu aina mbili, na hii ni ya mboga mboga a.k.a veggie soup
Halafu kulikua na nyama ya ng'ombe ya kukaangwa
Wakanikumbusha T.bonas nlipoona jiko na uwepo wa kuku choma
Kulikua na kuku waliopikwa kwa mchuzi .a.k.a chicken curry
Halafu kulikua na nyama ya ng'ombe iliyoungwa na mchicha na tui la nazi
Kulikua na nyama ya kondoo, ambayo nayo ilipikwa huku ikiwa na rojo
Nyama iliyokaangwa nayo ilikuwepo tayari kabisa kuliwa na wageni
Kulikua na kisamvu kilichoungwa na tui la nazi
Viazi vya kukaangwa navyo vilikuwepo, lakini sio katika mtindo wa chipsi
Shughuli haikamiliki bila ya mchele kuwepo, wali mweupe ulikuwepo pia
Halafu kukawa na wali wenye mbogamboga a.k.a veggie rice
Vikoromwezo lazima viwepo ili kukamilisha utamu wa menyu nzima
Kwanza kulikua na green salad
Salad ya veggies na mayai ya kuchemshwa nayo ilikuwepo
Kukawa na ile ya viazi vilivyochanganywa na mayonnaise, pembeni imerembwa na vipande vya matikiti maji
Kiukweli meza ilipendeza mno, kutoka upangaji hadi ladha ya vyakula vilivyokua vimeandaliwa kusindikiza hiyo siku ya Samsung pale hoteli ya Golden Tulip iliyopo Masaki.
No comments:
Post a Comment