Monday, November 5

Samsung week - Golden Tulip!!

Wiki iliyopita ilikua ni wiki maalum kwa kampuni ya Samsug, kwani walikua wakiuza bidhaa zao katika bei ambayo ni njema kabisa na inayoweza kuwafanya watanzania wapate fursa ya ununuzi wa bidhaa nyingi za nyumbani na makazini kwa bei maalum.
   Shughuli ya Ijumaa ilianza mapema, ila Menu Time ilihudhuria mwaliko wa chakula cha usiku. Nakujuza kwa phases jinsi shughuli ilivyokwenda, na haswa kwenye upande wa chakula. Karibu ujionee yaliyojiri.
   Ukifika wapokelewa na kibao kinachokuonesha wapi sherehe inafanyika
 
  Ukifika mlangoni wapokelewa na wadada wenye tabasamu bashasha na nyuso za furaha kuonesha kwamba usiku wa leo, mengi mazuri yatatokea. Mlangoni mahudhurio huchukuliwa, kisha wapewa namba ambayo itashindanishwa baadae kwa mchezo wa bahati nasibu, kuweza jishindia zawadi kedekede.



   Wakati tunasubiriana, ili shughuli ianze, kulikua na bites zinapitishwa na waalikwa tulikua huru kujisevia. Picha zifuatazo zinaonesha bites zilizokuwepo:

 
   Sasa wale wapendao nyama nao walizingatiwa uwepo wao, kama inavyojionesha kwenye picha, kuna meat rolls.
 
   Pia mishkaki ya ng'ombe ilikuwepo
 
    Hapo ni mwanzo tu, yaani tulipoingia kwenye hiyo shughuli ndivyo tulivyopokelewa.

No comments:

Post a Comment