Friday, September 21

Umuhimu wa Maji mwilini.....inaendelea

   Bado tunaendelea kukujuza na kukuelimisha umuhimu wa maji mwilini.
   Tulisema kuwa tuwe tunakunywa si chini ya bilauri mbili kwa siku. Wataalamu wanasema tunywe lita mbili kwa siku. Kama hatukuwahi kuwa na mazoea ya kunywa maji kwa kiwango hicho mwanzo huw ni mgumu, lakini waweza anza mdogo mdogo kwa bilauri mbili, kesho yake tatu, inayofuata nne mpaka tufikie hizo lita mbili.
   Kuna wale wenzangu na mimi watakaosema maji hayana ladha, nakupa maarifa kidogo waweza changanya na kikorombwezo upendacho kuyapa ladha ili upate hamu yakuyanywa, maana mwisho wa siku ni lazima kunywa maji, Waweza tumbukiza kijipande cha ndimu, au chungwa au kitu kingine unachopenda ladha yake

 
   Umuhimu wa Tano wa maji mwilini ni kwamba, unywaji maji hupelekea kusafisha ngozi yako, na mara kwa mara Rafiqs wengi wamejivunia kuwa na ngozi bora baada ya unywaji wa maji wa kutosha. Haiwezi tokea mara moja ila baada ya wiki moja utaanza kuona mabadiliko ya ngozi yako na itaanza kung'ara.
   Sita, mfumo wa kuchanganya chakula ndani ya miili yetu (digestive system) unahitaji maji mengi ili kufanikisha kazi yake kifasaha, hivyo yatupasa kuhakikisha mfumo huo unafanya kazi yake vyema katika muda sahihi kwa kunywa maji ya kutosha. Pia maji husaidia kuponesha maumivu ya vichomi vya tumbo, na pia hutupa urahisi pale tuendapo haja kubwa, kwani tunakua hatuna ukosefu wa maji mwilini. Maji husaidia pia kuondosha uchafu ndani ya miili yetu na kuacha mwili ukiwa msafi.
   Saba, Kwa unywaji mwingi wakati wa mfumo wa kuchanganya chakula unaendelea, imeonekana kuwa maji husaidia kupunguza uwezekani wa kupata saratani ya colon kwa asilimia 45, asilimia 50 ya saratani ya kibofu cha mkojo na pia hupunguza uwezakano wa kupata saratani ya matiti kwa kina mama.
  Nane, Kuwa na ukosefu wa maji mwilini husababisha kukurudisha nyuma katika swala zima la mazoezi na kukufanya iwe ngumu kunyanyua vyuma vya mazoezi, pamoja naa kufanya mazoezi mengine, hivyo basi inashauriwa kunywa maji kabla, wakati na baada ya mazoezi ili uweze kuyafanya vyema na katika hali salama.
   Tumemaliza kuongelea umuhimu wa Maji mwilini, iwapo kuna lolote tumeliacha basi karibu utufahamishe kwa kupitia info@menutimetz.com nasi tutarejea hapa na kuwajuza wenzetu.
Kifuatacho MenuTime ni kuongelea ni namna gani Rafiq mnaweza kutengenea mazoea ya kunywa maji ili sote tuweze kunywa maji inavyoshauriwa na wataalamu.
  Timu ya MenuTime inawatakia Ijumaa Kareem.

No comments:

Post a Comment