Thursday, September 20

Umuhimu wa Maji mwilini

   Tunaambiwa kuwa maji ni muhimu sana ndani ya miili yetu. Maji yana faida nyingi sana na wengi tunazijua, lakini tutajikumbusha baadhi. Tuanze hivi, Moja maji husaidia kupunguza calories mwilini, yaani badala ya kunywa vimiminika vingine kama soda, bia na juisi ambavyo vina calories, maji hayana calories. hivyo utakua umekunywa maji ambayo ni salama mbadala na vinywaji vingine ambavyo vina calories.Kumbuka pia maji hayana sukari, mafuta na viungo vingine vinavyotengeneza vimiminika vingine

   Pili, unywaji wa maji mengi hutupunguzia uwezekano wa kupata magonjwa kama ya moyo, hivyo inashauriwa kwa siku tunywe zaidi ya bilauri mbili za maji na kuendelea. Tatu, maji huongeza nguvu mwilini kwani unapokua na upungufu wa maji, unaanza na kusikia kiu ambayo huenda kupelekea kujisikia uchovu, misuli kuchoka, kizunguzungu na ishara nyingine za kunyongonyeza mwili.
  Nne maji ni dawa ya maumivu ya kichwa. Mara kwa mara tuumwapo kichwa pengine ni upungufu wa maji ndio uliopelekea maumivu haya, lakini tunywapo maji basi maumivu huoondoka. Kuna sababu nyingine zinazopelekea vichwa vyetu kuuma lakini, ukosefu wa maji mwilini ni sababu inayojulikana zaidi.
   Iwapo unajua faida za kunywa maji mengi, na hasara za upungufu wa maji mwilini, tuandikie kupitia
info@menutimetz.com.
   Tutaendelea kuwafundisha umuhimu wa maji mwilini, endelea kututembelea
.

No comments:

Post a Comment