Wednesday, September 19

Snack - Kula kula tyme

   Leo ni moja ya zile siku ambazo mmoja wa wana menu Time hajiskii kuingia jikoni kabisaaaa, sio kwamba sijiskii kupika mda mrefu, laaah. yaani hata kukoroga yai naona uvivu!!
   Ndio inavyokua kuna siku unakua na hamu ya kupikia watu karibia elfu na.... , na siku nyingine kama leo. Basi wakati najirejesha kwangu, baada ya mihangaiko ya siku nzima nkaona isiwe shida, nikatize kwa ndugu zangu nikajibebeshe vijisnack
   Kachori, Bajia, Samosa,Kalimati sijui na vikorokoro gani huwa mara nyingi navila kwa hamu, haswaaa pale napokosa hamu ya kupika.
   Tuliwahi kuongelea K-tea shop ambayo yajulikana sana, ila leo kuna kona ingine, watoto wa mjini wanaita chaka lingine, nimegundua. Angali walichonacho afu nkujuze zaidi hapo chini

 
   Kwa kawaida hao Rafiqs wana kachori, bajia, miksi na vinginevyo, yaani mwenzenu huwa navikumbuka hivi kwasababu ndo navovinunua mara kwa mara nikifika hapo.
   Nikujuze wapi wapo, Wapo mitaa ya Upanga uhindini kule, nakuelekeza ukianzia kituo cha mabasi kiitwacho aga khan, kile kama waenda mwenge, sasa kabla hujafika si kuna kona ya kueleke kwa kuku wekundu restaurant, fika mpaka mwisho wa barabara afu pinda kushoto mbele kidogo mkono wa kulia wapo wamesimama kwenye kijinjia cha kwenda ghorofani kwa wenye nyumba. Basi hapo unatoa oda wanakupatia fasta vya motoooo, sahani ya bajia buku mia tano, wataka nini sasa navyo vinakaa kumi.
   Kikorombwezo cha chetna wanakupa bureeeee na ndimu ka wataka kuongeza nakshi kwenye ladha. Glass ya wine na vijimatunda vya strawberry vinajitegemea vyenyewe.
  Kama una sehemu ingine wanapika na kuuza snacks, basi tujuze nasi tukavionje na kuwajuza wengine, Hii ndio Menutime, kazi yetu ni kutangaza chakula.

No comments:

Post a Comment