Saturday, September 22

Namna ya kujenga mazoea na tabia ya kunywa Maji

   Tumeangalia umuhimu wa maji mwilini katika siku mbili zilizopita, na tumeona faida nyingi za unywaji wa maji. Sasa baadhi yetu hatuna mazoea ya kunywa maji mara kwa mara, Menu Time team ikaona ni vema tukishare nanyi namna ya kujenga mazoea au tabia ya kunywa maji mara kwa mara ili kufikia kile kiwango ambacho utakua umejiwekea.
Karibu....


   Cha kwanza tujiulize, kiasi gani cha maji twatakikana kunywa? ilivyoshauriwa ni bilauri nane kwa siku,??? Inawezakana sio sahihi...... kwasababu kiasi hicho kinahusisha maji safi ya kunywa tunayoyanywa, pia maji yanayopatikana kwenye vyakula tunavyokula na vinywaji vingine mbali na maji ya kunywa. Pia kiasi hiko hakikuangalia uzito wa miili yetu kitu ambacho ni muhimu sana tunapoongelea kiasi cha maji cha kunywa, na kingineeee kiasi cha maji hutofautiana pale ambapo tunaumwa, au kwa wale tunaofanya mazoezi kila siku.    
   Kingine unaposikia kiu, kumbuka kwamba tayari una upungufu wa maji kwa hiyo kunywa pale hakuhesabiki katika zile bilauri nane za kunywa maji.


   Cha kufanya basi, ni kujenga mazoea: kunywa bilauri moja ya maji pale uamkapo, bilauri moja kila baada ya mlo, bilauri moja katikati ya milo yako ya siku, na kumbuka kunywa maji kabla, wakati wa na baada ya mazoezi. Jaribu kuepuka kupata kiu ya maji.
   Cha pili, beba chupa ya maji: Wengi wenye shughuli za kutembea hapa na pale itawapasa kubeba chupa ya maji mkononi na kunywa mara kwa mara, inapoisha ongeza ingine. Na kwa wale wanaokaa maofisini, weka bilauri ya maji pembeni yako na uwe unakunywa mara kwa mara na kuongeza pale inapokwisha.
   Njia nyingine,ni kuegesha mlio kwenye saa ya mkononi au ya kwenye simu, au kwenye Computer yako, iwe inalia kila lisaa kamili linapotimu, ili uweze kukumbuka pale unaposikia kengele au alarm.
   Iwapo unajisikia hamu ya kunywa soda au kimiminika chenye kilevi au cha aina nyingine yeyote, badala ya kukifuata hicho, badili na fuata bilauri ya maji na uinywe. Jaribisha maji yenye ladha pale unapokua katika sherehe au makutanoni na marafiqs.
    Anza mazoezi, kwani mazoezi hukufanya uwe na hamu ya kunywa maji maana si utasikia kiu. Si lazima kunywa vinywaji vya kuongeza nguvu, ila kama unafanya mazoezi zaidi ya lisaa limoja na kuendelea waweza kuvinywa. Kunywa maji mapema iwapo wajua utaenda kufanya mazoezi, kwani itasaidia maji kufika kwenye system ya mwili wako vyema pale unapoanza mazoezi, kunywa maji wakati wa mazoezi na baada ya mazoezi.
   Fuatilia mwenendo wako wa unywaji maji kwa kuandika pahala kwa ajili ya kumbukumbu. Hii itakusaidia kukuonesha na kukukumbusha kwamba yakupasa kunywa maji katika muda ule ule kila ufikapo na kiasi ambacho umejipangia. Andika muda upande wa kwanza na wapili unaweka alama ya vema kila mara unywapo maji.
   Iwapo una njia nyingine mbadala na hizo hapo juu, tujuze kupitia info@menutimetz.com nasi tuweza kushare na Rafiqs wote wa MenuTime.
   Menu Time team inawatakia Jumamosi na Sabato Njema!!!

No comments:

Post a Comment