Sunday, September 23

Breakfast picha toka Marekani

   Mmmmh swala la Kifungua kinywa a.k.a breakfast lina umuhimu kwa kila mmoja wetu katika kuanza siku. Kuna wale Rafiqs ambao tunda moja au bilauri ya juisi/ maziwa inawatosha kabisa kuanza siku. Well, wana sababu zao zinazowapelekea kufanya maamuzi hayo.
  Halafu kuna wale Rafiqs ambao menu lazima iwe ya kutosha maana tunaweza pitisha mchana dry, yaani fresh tu maana tumefungua kinywa na kilo kadhaa za msosi.
  Kutoka Marekani, mji sikuulizia saaana, Rafiq ameshare nasi moja ya siku aliyoamua kufungua kinywa katika uhakika wa kuanza siku vyema

 
     Naona kuna mikate iliyookwa, jicho la ng'ombe, sausages, afu kama kachumbari nadhani, sina hakika ni nini hichi upande wa chini. Ameshushia na nini, hakutuarifu ila naamini maziwa au chai au hata juisi inashuka vyema kabisa.
     Tujuze wewe unaanzaje siku yako, tutumie kupitia info@menutimetz.com au menutime@menutimetz.com nasi tutashare na Rafiqs wengine wote watembeleao blog yetu.
    Peter, shukrani sana kwa kushare nasi your breakfast!!
 Team ya Menu Time inawatakia Jumapili njema yenye Baraka!!

2 comments:

  1. Huyu mdau lazima alivimbiwa. Maana hash brown na hizo french toast... Msaala!-George,T.Bonaz

    ReplyDelete
  2. Heheeeeee, Peter said amekula mwenyewe yooote, na alishushia na hot chocolate!!

    ReplyDelete