Sunday, September 16

Menu Time team @ Ilala

   Wana MenuTime wakaona leo waamkie maeneo ya Ilala kwa Meck Sadiki, kujipatia kifungua kinywa. Hatuongelei nyumbani kwake laaaah, bali hili si ndo jiji lake???? nasi tupo kwake. Tunaongelea muda huu tunaporusha post hii, yaani sasa hivi!!

 
    Bar yajulikana kama Miami bar na ukifika tu, ulizia kwa bonge au da Mary basi utapata huduma safi kabisa!!. Karibu kufungulia kinywa hapa na supu ya pande yaani ya vipande vya mbuzi, halafu kuna supu ya kichwa, kuna chapati na mengine mengi hatuezi malizia uhondo kwa kuyataja yote.
   Fika Ilala uonje!!
Menu Time team we signing out!!
   

No comments:

Post a Comment