Sunday, February 26

Mapishi ya kuku toka Marekani

   Kutoka Marekani, tumepokea email ambayo rafiq yetu Catherine ametutumia akionesha alivyopika kuku, ambapo mapishi yake aliyatoa humuhumu MenuTime blog, katika post za Mapishi time, ya tarehe Friday, January 13, 2012. Kichwa cha habari kinasomeka  "kuku wa kurosti na viazi" ambapo upishi wake alitujuza Da Mage na MenuTime ikapika na kushare hatua za upishi pamoja na picha.
       
   Bi Catherine, amepika kuku wake na hizi ndio picha zake:


 Alisema aliongeza nyanya ili kupata ladha anayoitaka yeye, na kwa hapo amenipa ushawishi wa kujaribu hili pishi lake na muongezo wa nyanya.

Kusindikiza mlo huu alitengeneza viazi vitamu pamoja na njegere.

 Huu ndo ujumbe aliotuandikia ukiambatana na picha zote hapo juu:
"Hi Lulu,
I trust all is well with you.
As promised, here is my version of the "rost chicken" as submitted by a reader of your blog. I added tomatoes to it since I wanted it more moist; also served it with baked sweet potatoes and sweet peas sauce. Served 2 tummies, and must it was scrumptious....got plenty of compliments on the chicken...lol
Again, many thanks for everything, keep up the good stuff"

Asante sana Catherine.

No comments:

Post a Comment