Sunday, January 8

Menyu kutoka Hotelini ya Wachina - Dar iliyo Salama!

    Kuna baadhi ya siku ambapo hutaki kuingia jikoni na unaamua kwenda kujipatia mlo wa mchana, usiku na hata wa asubuhi mgahawani, hotelini, restaurant na kadhalika.
   Moja ya sehemu nilizotembelea wiki hii hapa Dar iliyo salama, ni Great wall Restaurant ambayo ipo Oysterbay,barabarani kabisa na kama unatokea St. Peters, utaiona upande wa kulia kabla ya kufika Jackies bar.
   Ni restaurant ya wachina, mpya mpya haina muda saaana, ni nzuri ndani na nje, mandhari nzuri, wahudumu wapo fasta na menyu yao ipo safi.

Nilianza na supu, na niliagiza ya mbogamboga a.k,a vegetable soup


Nilikua na njaa ya kutosha mie na Rafiq yangu, so tukaagiza prawn noodles, vegetable rice, na sweet and sour chicken.
Hii potion unayoona hapo ndo tuliagiza watu wawili, ila mnaweza kula hata wanne na mkashiba vyeema.
Kama upo Dar, na unataka kula vya wachina hii ni restaurant ya kutembelea. Kama utawahi kuja Dar usisahau kupitia hapa na wewe upate utamu wa mapishi ya wachina.

Kama kuna sehemu inatoa huduma safi ya menyu na ungependa sote tujue, basi tuletee khabari zake kupitia menutimes@gmail.com nasi tutawatembelea.

Kutoka Great wall Restaurant, LJM naarifu.

No comments:

Post a Comment