Monday, January 9

Menyu ya Hotelini

  Mie binafsi moja ya vyakula napenda sana ni kamba a.k.a Prawns pamoja na tambi a.k.a macaroni/pasta. Ukiondoa zile napika mwenyewe, nikienda Hotelini mgahawani au sehemu ya vyakula nakua mrahisi kutoa order hiyo ili nione wao wanapikaje????
   Sehemu nyingine nilipata kutembelea ni Karambezi Cafe iliyopo Sea cliff hotel kulee Masaki dar iliyo Salama. Nilikua na familia tunapata chakula cha jioni.
   Mara nyingi ndugu zangu wao wanapenda nyama ya nguruwe na iwapo haitakutwa hiyo basi Tbone steak ndo inafuatia.

   Menyu hii ilitafunwa na dada yangu: Tbone steak well done pamoja na viepe
Hapa niliharakishwa kupiga picha kwani alikua na njaa muno. Basi fasta fasta ndo mpango mzima ukatokea hivyo.

Hii niliagiza mie, chilly pasta with prawn & loads of cheese

 Hakika menyu ilikua tamu kama inavoonekana hapo juu. Lazima niseme hudumu katika mgahawa huu imepanda sana yaani ni nzuri mno, wahudumu wapo fasta na order inakuja fasta katika meza yako.
Sasa kama upo maeneo ya masaki hapa dar iliyo salama, mie nakushauri upitie hapo upate mlo wa mchana hata wa usiku na kama sio mida hiyo umepita hapo, basi japo unywe kahawa mwenzangu upate hudumu nzuri.

Kutoka Karambezi cafe, iliyopo Sea cliff Hotel, LJM naarifu.

No comments:

Post a Comment