Tuesday, January 10

Karibu sokoni a.k.a Shopping

   Tuliahidi kwamba tutawajuza wapi mnaweza pata mahitaji mbali mbali na kwa bei ipi. Tunaendelea kulifanyia kazi hili kwa umakini na utaratibu na mwisho wa siku sote tuweze kujua wapi tutapata baadhi ya mahitaji yetu kama si yote katika kupika menyu zetu.
   Jana tuliwatembelea hawa ndugu zatu wanaitwa Home Butchery Limited. Tumeamini jina lao kwa sababu humo unapata nyama za aina zote kuanzia kuku, kamba, ng'ombe, mbuzi, samaki, nguruwe, kondoo, sausages, nyama choma n.k yaani wewe tu na nyama uitakayo.
  Halafu wanakupa ushauri, yaani we unawaelezea unataka nyama ipi ili ukapike nini, nao wanakushauri kutokana na uzoefu wao.
   Ukutani nilikutana na picha hizi:


  Kingine tumependa ni kwamba, ukitaka nyama ambayo tayari imeshatiwa nakshi za viungo vyote a.k.a marinated wanakua nayo tayari.Watembelee upatapo nafasi....

Home butchery Limited wanapatikana Nkrumah Street,
Simu: +255 22 2111692
Cell: +255 713 324731

  Kama unatokea mjini ukishapita clock tower, unapita Club continental pande ya kulia, mbele kidogo upande wa kushoto baada ya sheli, utawaona.

Kutoka Nkrumah street, MenuTime inawaarifu.

No comments:

Post a Comment