Friday, January 13

Mapishi ya Kuku wa kurosti na viazi

  Swahiba wangu Megvictor Mashobe, Mke wa rafiq yangu ambae anaujuzi mzuri wa kupika aina mbalimbali ya vyakula ndiye aliyenifunza namna ya kupika menyu hii.
  Huyu kuku anaweza kuwa wa kienyeji au wa kisasa, inategemea na wepesi wako wapi unampata. Ila kitakachotofautiana ni kwamba kama una kuku wa kienyeji, basi muda wa kumpika jikoni utakua mrefu zaidi kuliko muda wa kumpika kuku wa kisasa.
 
 Mahitaji:
  • Kuku mzima mmoja
  • Kitunguu maji kimoja
  • Kitunguu swaumu kilichotwangwa
  • Tangawizi moja iliyotwangwa
  • Pilipili manga iliyoswagwa
  • Chumvi kiasi
  • Viazi
  • Mafuta ya alovera

    Hatua:
    • Katakata kuku wako katika vipande upendavyo, vyaweza kuwa na ukubwa kiasi au vidogo vidogo zaidi
    • Weka kwenye sufuria, ongeza kitunguu swaumu na tangawizi zilizotwangwa, ongeza chumvi kiasi na pilipili manga.(Waweza weka ndimu na pilipili kichaa bila kuikata kama unapenda)
    •  
    • Washa jiko na weka sufuria lenye mchanganyiko huo, acha utokote kwa muda
    • Ongeza maji kidogo kila unapoona kama unakaukia kwa sufuria
    • Ili kuokoa muda menya viazi vyako
    • Katakata ukubwa uupendao, kama ni size ya chipsi au vikubwa kidogo sawa tu kwa mapenzi yako
    • Katia vitunguu maji, ongeza chumvi kidogo na kisha bandika jikoni
    • Chemsha kwa dakika chache, kisha vigeuze kwa kupepeta, acha viive kidogo kisha epua, ondoa maji na weka pembeni
    • Chukua kikaangio chako weka mafuta na kaanga viazi vyako tayari kwa kuliwa
    • Kuku akishaiva muepue na muweke pembeni
    • Weka kikaango jikoni, ongeza mafuta kidogo, chumvi na vitunguu maji vilivyokatwakatwa
    • Vitunguu vikishaiva na kugeuka rangi, ingiza vipande vya kuku na vikaange kwa muda,(Waweza ongeza nyanya kama utapenda)
    • Epua kuku wako tayari kwa kuliwa
     
    Nilipenda zaidi na chipsi, ila waweza kula na chochote hata ndizi choma.Kizuri waweza jiongezea na kachumbari kidogo na vinginevyo kama mayonnaise, chilli sauce na kadhalika
    Jaribisha halafu tujuza kupitia menutimes@gmail.com usisahau na kaushaidi ka picha.
    Bi Mage asante sana kwa kutupa pishi la ukweli.

3 comments:

  1. umenichanganya hapo baada ya kukatakata viazi - umesema unachemsha "viazi" pamoja na vitunguu? tafadhali saidia kufafanua ama kuweka clearer..
    Asante
    MJ

    ReplyDelete
  2. Rafiq, hapa hapakuelezewa namna ya kupika viazi. Ila kwa kujua namna ya kuchemcha viazi kwa vitunguu ni kwamba, baada ya kukatakata viazi vyako na kuviosha, unaweka kwa sufuria na maji kiasi kisha waweka chumvi na vitunguu maji vilivyokatwakatwa. Sababu ya kuweka vitunguu maji ni kuongeza ladha kwani viazi vikichemshwa pekee na chumvi tu haviwi ni ladha ya ziada.
    Pia kitunguu maji kina faida kwa miili yetu mojawapo ni kusafisha mwili ukiondoa kuongeza ladha

    ReplyDelete
  3. da asante kwa pishi hili nitalipika kwa kuku wa kienyeji

    ReplyDelete