Wednesday, January 4

Mapishi ya tambi na vipande vya kuku visivyo na mfupa

Mara nyingi mwenzenu naona kama kupika tambi a.k.a macaroni ni rahisi mno, na kama sitaki kuwepo jikoni kwa muda mrefu, basi huo ndo mlo napenda kuupika. Upande wa mboga, well yeyote yaweza kuwa mbogamboga bila nyama, sausages, nyama ya kusaga, nyama ya kuku na kadhalika, yaani ni utundu na ufundi wako wewe mwenyewe.
  Katika sikukuu hizi zilizopita, moja ya menyu tuliyopika ni hii ya tambi na vipande vya kuku visivyo na mifupa a.k.a boneless chicken.
  Hawa wanapatikana kwenye supermarkets ila waweza kununua fresh, ukachinja, nyonyoa, halafu ukatoa minofu pembeni na mifupa pembeni.... ubunifu wako tu, mwisho wa siku uwe na hao kuku wasio na mifupa. Upo tayari? Twende sasa.....

Mahitaji:
  • Kuku mzima asiye na mifupa
  • Kitunguu swaumu
  • Kitunguu maji
  • Tangawizi
  • Chumvi kiasi
  • Nyanya 2
  • Tui la nazi
  • Jibini
  • Tomato puree
  • Sauce ya tambi (chagua ladha uipendayo - zinapatikana Supermarkets)
  • Tambi
  • Pilipili manga
  • Maji safi

Hatua:
  • Chukua sufuria safi, weka maji kiasi, ongeza chumvi kidogo na pilipili manga iliyotwangwa
  • Weka jikoni na wacha yachemke
  • Ongeza tambi zako ndani ya maji na acha ziive kwa muda wa dk 10, (tafadhali onja tambi kama zimeiva vyema)
  • Zikisha iva, epua tambi, zichuje kisha mwagia maji baridi
  • Rejesha kwenye sufuria ongeza blueband kidogo huku unayakorogakoroga
  • Tambi zako zipo tayari kwa kuliwa
  • Tuanze na mboga, weka sufuria safi jikoni, ongeza mafuta kiasi na yaache yachemke
  • Ongeza chumvi kidogo, ongeza vitunguu maji vilivyokatwakatwa na vitunguu swaumu natangawizi zilizopondwa
  • Mchanganyiko huo ukiiva vyema ongeza nyama ya kuku isiyo na mifupa, pamoja na viungo pendavyo wewe
  • Baada ya kuku kuiva vyema na kugeuka rangi ya brown kidogo, ongeza nyanya na acha vitokote
  • Ongeza tomato puree ili kufanya mchanganyiko uwe mzito vyema
  • Ongeza sauce ya tambi (uipendayo ladha yake) kisha acha mchanganyiko huo ukolee vyema
  • Malizia na tui la kwanza la nazi, ukiisha liweka koroga mboga yako na hakikisha haichemki kwani tui litakatika
  • Epua mboga yako, chukua chombo kikubwa zaidi weka tambi zako, changanya na mboga yako (weka kidogokidogo huku unakoroga mchanganyiko huu ili ukolee vyema)
  • Chombo hicho hakikisha kiwe na uwezo wa kuwekwa jikoni yaani sio plastic
  • Chukua jibini yako (yaweza kuwa ya maji, au ya kukatakata au kukwaruzwa - zinapatikana Supermarkets) na changanya vyema na mlo wako ukiwa jikoni lakini katika moto mdogo ili jibini iyeyuke vyema ndani ya mchanganyiko wa tambi na nyama ya kuku.

Menyu yako ipo tayari Rafiq, Karibisha marafiq, familia, wageni tayari kwa menyu,,,,,,,, ya kwetu  ilitokea hiviii:



Kama kuna swali, au wataka kujuzwa zaidi kutupata tafadhali bofya hapo contact us, Laa, tuandikie kupitia menutimes@gmail.com nasi tutakurejea.

Toka Menu Time team tunawatakia Kheri ya Mwaka Mpya 2012!!!

4 comments:

  1. sio ongeza, sema weka..

    ReplyDelete
  2. Rafiq, shukrani kwa kutusahihisha, lakini si tulieleweka???

    ReplyDelete
  3. Rafiq, shukrani kwa kutusahihisha, lakini si tulieleweka???

    ReplyDelete
  4. Asante sana kwa mapishi mazuri. Leo hii naenda kujaribu! Weka na ongeza yote sawa hakuna tofauti. Huyo mtu anataka kukuzengu tuu boss.

    ReplyDelete