Thursday, December 22

Mapishi ya Ugali na KUKU wa Kubanikwa

Tunaende kwenye sherehe za Noeli a.k.a Krismas na za kufunga mwaka a.k.a. Mwaka mpya. Na hapa ndio ndugu mbalimbali tunakutana na marafiki, majirani tukisherekea, tukipongezana na kutakiana afya njema katika kuanza mwaka mwingine.
Menu Time tupo nanyi katika sherehe hizi na tutaendelea kuonesha aina mbalimbali za vyakula ambavyo tutapika, tutakutana navyo, mtatutumia na tunaamini mtaweza nanyi kujaribu kuvipika.
karibuni katika mapishi ya Ugali na Kuku wa kubanikwa.

Mahitaji:
  • Kuku mzima mmoja
  • Kitunguu kimoja
  • Karoti moja
  • Pilipili hoho moja
  • Ndimu moja
  • Chumvi kiasi
  • Kitunguu swaumu kiasi
  • Tangawizi kiasi
  • Viungo vya pilau kiasi
  • Unga wa mahindi
  • Maji safi ya kupikia
 Hatua:
  • Katakata kuku vipande vya wastani (hakikisha kuku amenyonyolewa)
  • Twanga vitunguu swaumu + tangawizi kisha weka pembeni
  • Kamua ndimu changanya na vitunguu swaumu na tangawizi na viungo vyapilau ( kama kuna ladha ingine ungependa ongeza, waweza fanya hivyo mathalani asali, siki a.k.a vinegar n.k
  • Changanya vipande vya kuku na mchanganyiko wa ndimu na viungo kisha acha mchanganyiko huo kwa dk 30 ili viweze kukolea vyema
  • Katakata pilipili hoho na karoti weka pembeni
  • Tayarisha tray ya kubanikia kuku wako kwa kuipaka mafuta ya kupikia
  • Weka pilipili hoho na karoti
  • Weka kuku wako ambao wamechanganyika na viungo katika bati la kubanika
  • Ingiza ndani ya oven yako na waache waive kwa dakika 45, kisha chungulia kama wameiva
  • Baada ya kuivisha ugali wako, weka mboga za majani kidogo na menyu itakua hivi;
  • Ukifanikiwa kupika kama hii piga picha na tutumie: menutimes@gmail.com

4 comments:

  1. hii nimeipenda. ntajaribu kutengeneza na Ugali. asante kwa recipe.

    ReplyDelete
  2. Tunashukuru kwa kupenda mapishi hayo. Tafadhali tujuze baada ya kuyajaribu. MenuTime Team

    ReplyDelete
  3. Kaa chonjo picha inakuja

    ReplyDelete