Vitumbua vina kikaangio chake maalum, na sio kwenye kikaangio cha kawaida. Ule muonekano wake watokana na shape ya kikaangio chake.
Kama nilivyosema nilimkuta tayari keshaanza mapishi, kuna nafasi sehemu moja tu ya kikaangio
Mafuta yanaongezwa kidogo, ili kitumbua kisije kukaukia kwenye kikaango
Na kwa shilingi 100/= tu za kitanzania unapata Kitumbua chako, ukishushia na chai , siku inaanza vyema. Vitumbua vyaweza kuliwa muda wowote sio lazma asubuhi tu. Wengine hupenda kuweka kuwa moja ya mlo wa sherehe.
Nilipokwazika mie, ni kutokuwa na kawa au mfuniko flani kuweza kuvitunza katika sehemu salama zaidi. Ila tulizungumza, alikubali kuandaa kijisanduku cha kuuzia vitumbua vyake.
Karibu kutoa maoni yako, tuma barua pepe kupitia menutimes@gmail.com
No comments:
Post a Comment