Karibu....
Kutengeneza pancakes nilitumia unga wa ngano, maziwa, mayai, chumvi kidogo, sukari kidogo:
Changanya unga wa ngano kiasi kutokana na mahitaji yako ya kutengeneza pancakes ngapi, mayai, chumvi kidogo, maziwa na sukari kidogo kama picha inavyoonesha.
Ushauri wangu ni kwamba katika kuchanganya tumia mwiko wa mbao
Tayarisha kikaangio a.k.a frying pan, ongeza olive oil kidogo na butter kidogo, tayarisha moto kiasi na sio mwingi kuepusha pancakes kuungua
Weka kiasi cha mchanganyiko kwenye kikaangio chako:
Baada ya dakika kama 2 hivi, Geuza upande wa pili ili nao uive vyema
Pancake yako ipo tayari kwa kuliwa.
Sausages nilizikaanga:
Mayai pia nilikaanga huku nayakoroga.
mwishoni Kifungua kinywa kilitokea hivi: ya kwanza ni yenye pancakes:
Ya pili ni yenye mikate ya kuchomwa a.k.a toasted bread mmmmmmmh
Waweza kushare nasi Kifungua kinywa chako kwa kututumia kupitia menutimes@gmail.com Karibuni sana!!
No comments:
Post a Comment