Friday, August 1

Kilimanjaro, Moshi

  Badi tupo Kilimanjaro, Moshi na tunaendelea kuwajuza menu mbali mbali tunazozipata huku, na bado tupo Weru weru lodge tulipofikia.
  Jana jioni tulipishana na watalii wengi waliotoka na waendao kupanda mlima mrefu Afrika, tunaongelea mlima Kilimanjaro uliopo hapa hapa Moshi, Kilimanjaro, Tanzania.
  Waliotoka kuupanda walikua na kila sababu ya kusherekea kutimiza lengo lao na vinywaji vya mlipuko a.k.a champagne vilisikika kufunguliwa kila kona ya meza kusherekea utimizaji wa lengo lao la kupanda mlima mrefu Afrika, mlima Kilimanjaro.
  Wakati wanafurahia hayo, huku wengine wakiwa na shauku ya kwenda kuupanda, wana Menu Time tukajiuliza, ivi je itakuaje na sisi tukiamua kuupanda? Tujuze kama utapenda kuungana nasi iwapo hilo shauri litapendekezwa na kupita.
  Chakula cha usiku tulipata hapahapa Weru weru lodge na udhibitisho ni huu hapa chini. Kama kawaida tulianza na supu
Ilikua ni supu ya mboga mboga, na pembeni tulichukua kipande cha mkate pamoja na salad, ili kulainisha tumbo kabla ya mlo kamili.

  Kisha tukaingia kwenye mlo kamili kama ionekanavyo hapo chini
  Mtindo wa usiku ilikua ni buffeet ambapo kulikua na aina mbalimbali za vyakula na kwenye sahani yetu tulichukua kabichi zilizokaangwa, kipande cha kuku aliyekaangwa na viungo, beef lasagne, kabab za samaki, viazi vilivyookwa pamoja na ugali uliopikwa kimexco yaani una maziwa na cheese.
   Tulishushia na glasi ya mvinyo mwekundu na kushukuru siku imemalizika vyema.
 Tutarejea kuwajuza zaidi kuhusu menu nyingine tutakazozipata bado tukiwa hapa.
  Kutoka Kilimanjaro, Ljm naarifu!!

No comments:

Post a Comment