Thursday, July 31

Kilimanjaro, Moshi

   Asubuhi ya leo tumedamka na kuelekea nyumbani yaani Kilimanjaro, Moshi, na tutaishia Moshi mjini pasi kufika Rombo mkuu kwa bibi.
   Hoteli tuliyoshukia ni Weru weru Lodge ambayo ina mandhari nzuri mno, na utulivu wa hali ya juu.
  Mchana ulipotimu tuliagiza mlo kwa ajili ya kupoza njaa, na kujitoa na uchovu wa safari.

Rafiqs karibuni kushuhudia menu yetu ya mchana kutoka hapa
  Tulianza na supu yenye vipande vya kuku na uyoga, na kwa ushahidi pata picha hapo chini



Kwa mlo kamili tulipata kuagiza chipsi pamoja na nyama ya steak, vikisindikizwa na salad kidogo na sauce pembeni kwa ajili ya kuilia hiyo nyama
   

 Kutokana na hali ya ubaridi, tulipendelea kupata Cappuccino katika kusindikizia mlo huo, na hiki ni kikombe ambacho tulitayarishiwa
      

 Tutaendelea kuwajuza menu kadha wa kadha tutakazopata hapo, kadri ya siku tutakazoishi hapa.
Kwa kupata habari kwa uharaka zaidi tufwate instagram kupitia @menutimes pia twitter tunafwate kupitia @menutimetz na kwenye face book page yetu ni www.facebook/Menu time.com

No comments:

Post a Comment