Thursday, April 17

Usiku wa mwisho pande za Moshi

   Baada ya cha mchana, ilitupasa kula vyema cha usiku, kabla ya kurejea kwetu Dar iliyo salama, na kama ilivyo ada marafiqs wakatupeleka sehemu ingine ambapo mdudu yapatikana.
 Si unajua ukiwa msafiri, shurti ujaribu ladha toka maneo mbalimbali ya unapotembelea, basi hapo tulipokua habari ilikua hivi,
Ikiwa peke yake

  Na hapa ikiwa na ndizi pamoja na chachandu

    Eneo lajulikana kama Majengo, ulizia kwa Minja, na utapata utamu huo. Na leo ndo tumemaliza simulizi za safari yetu ya Arusha na Kilimanjaro.
   Kumbuka kesho ni Ijumaa kuu kwa wakristo, hairuhusiwi kula nyama. 
Tunawatakia kila la kheri katika wikiendi hii ndefu, pia kila la kheri katika sikukuu ya Paska!!

No comments:

Post a Comment