Wednesday, April 16

Cha mchana - Kuku maziwa

  Baada ya breakfast, tuliendelea na shughuli nyingine za kifamilia na kitaifa, na ilipotimu muda wa menu ya mchana, tulipelekwa sehemu maarufu kwa upishi wa kuku maziwa.
  Eneo lajulikana kama Kiboroloni ulizia Planet pub a.k.a Kuku maziwa.
Sasa wanavyoleta mezani, supu yenye maziwa inakuwa vibakulini, kisha nyama ya kuku tena wa kienyeji pamoja na viungo vingine kama ndizi na viazi vinawekwa kwenye sahani au sinia kutegemea na wingi wake.
   Karibu tuone, tuanze na huo mchuzi uonekanavyo

   Kisha maakuli yenyewe ndani ya sahani tayari kwa kushambuliwa

   Ukifika Moshi, fanya kupatafuta ili ukayajaribu mapishi haya yenye utaalamu tofauti. Muulize Dj Choka, kila aendapo Moshi haachi kupita hapo kwa ajili tu ya utamu upatakanao hapo.
   Mchana wetu ukaishia hapo, na hadithi inaendelea!!!

No comments:

Post a Comment