Monday, April 21

Menu za sikukuu ya Pasaka

 Kutoka Dar es salaam pande za Kivukoni pajulikana zaidi kama Mjini au Posta, kuna mjengo mpya waitwa VIVA complex, na Ground floor kuna mgahawa waitwa Rhapsody's, binafsi napaita taa ya blue kwa ajili ya decoration ya taa ziwakapo usiku.
  Mandhari ni nzuri, inavutia na pia huduma zake ni safi sana. Tulihudumiwa na bwana Salum na kwa kweli he was great Rafiq. Tunashea nanyi menu tulizopata hapo katika kipindi hiki cha Pasaka.
  Cha kwanza chajulikana kama Chilli Chicken Penne, ni kitamu ila tahadhari kina pilipili ya kutosha sana.

Cha pili ni Seafood pasta, ambapo kuna mchanganyiko wa kamba, ngizi na samaki pamoja na tambi.

   Ni sahihi kutumia pesa yako ukiwa pale, kwani mengi yatakufurahisha. Tunarejea kesho tena kuendelea kukujuza yalojiri. Tulikua familia nzima.

No comments:

Post a Comment