Friday, April 11

Machalari yaRombo Mkuu - Kilimanjaro

   Baada ya kufungua kinywa vyema, na mapokezi mengi, tukasema sio mbaya kwenda kusalimu bibi na wazee wengine kula tulipotokea, tunaongelea Rombo mkuu na Kilaracha.
   Ile kufika Rombo mkuu, tulikaribishwa na machalari yale ya kinyumbani kabisaa. Tukakaa kitako, tukala na kushushia na maji na kisha tukabeba zawadi kidogo, ili tukanywe mbele ya safari.
   Ushuhuda wa machalari tuliyokaribishwa nayo Rombo mkuu ni huu hapa

  Zawadi tuliyobeba kwa ajili ya kunywa tukiwa safarini ni mbege, ambayo ilipikwa vyema na iliiva vizuri. Kihalali mbege ilikua tamu mno, na muonekano wake ulikuwa hivi

  Wikiendi ndo imeanza, tunawatakia wikiendi njema, yenye amani na upendo na yale yote mnayopanga kufanya Inshallah mfanikishe. 
Tutarejea kuwaeleza tulichokula usiku kabla ya kufungua kinywa, kula cha mchana na kuaga Moshi.

1 comment: